Dar es Salaam. Droo ya raundi ya sita ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup msimu huu imezipa mchekea timu za Yanga, Simba, mabingwa watetezi Mtibwa Sugar na Azam ambazo licha ya kupangwa na vibonde, zitaanzia nyumbani.
Mabingwa wa kwanza wa taji hilo waliotwaa msimu wa 2015/2016, Yanga wataanzia nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini kukabiliana na mshindi wa mchezo baina ya Ihefu na Tukuyu Stars.
Ikumbukwe kuwa msimu uliopita, Yanga ilikutana na Ihefu FC katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo na kuibuka na ushindi wa penalti 4-3 jijini Mbeya.
Simba iliyotwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu wa 2016/2017 na kisha msimu uliopita kuondolewa kwenye hatua ya 32 na Green Warriors iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Pili kipindi hicho, nayo imepangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.
Mabingwa watetezi Mtibwa Sugar wenyewe watakuwa nyumbani Manungu Complex kuwakaribisha Kiluvya United.
Azam FC ambayo imekuwa na bahati mbaya kwenye mashindano hayo yenyewe pia itaanzia nyumbani kwenye uwanja wa Azam Complex jijini ambako itacheza dhidi ya mshindi wa mchezo baina ya Madini FC na Stand Babati.
Ratiba ya jumla ya mechi za hatua hiyo ambayo itachezwa kati ya Disemba 21, 22, 23 na 24 hii hapa ikijumuisha na namba ya mchezo husika.
55. Namungo vs Sahare/Deportivo
56. Geita Elect/ Kumuyange vs Kagera Sugar
57. Mtibwa vs Kiluvya United
58. Lipuli vs Laera/Mitumba
59. Stand United vs Ashanti United
60. Changanyikeni/Baga FC vs Coastal
61. Reha vs Zakhem/Mkamba Rangers
62. Majimaji vs Toto/gipco
63. Boma vs Njombe Mji
64. Pan Africa/ Villa Sqd vs Mwadui
65. Cosmo vs Green Warriors
66. Rhino vs Nyamongo/Bulyanhulu
67. Azam vs Madini/Stand Babati
68. KMC vs Prisons
69. Kili heroes/Forest vs Polisi tz
70. Majimaji R/moro kids vs Mbeya Kwanza
71. Geita gold vs Biashara United
72. R shooting vs Mucoba/might elephant
73. Yanga vs Ihefu/Tukuyu
74. Singida vs Arusha FC
75. Sharp striker/usalama vs Friends rangers
76. Dodoma vs Kasulu Stars/ home boys
77. Mufindi United vs Alliance
78. Mbeya City vs Mgambo Shooting
79. African Lyon vs Arusha United
80. Simba vs Mashujaa fc
81. La familia /area c vs Mawenzi Market
82. Mbao vs Dar city
83. Milambo/Stand Dortmund vs JKT Tz
84. Mtwivila/Livingstone vs Pamba
85. Ndanda vs Transit Camp
86. Kitayosce/african sports vs Mlale fc