Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Yanga; Kama vipi mmoja aongoze kundi halafu wakutane Robo Fainali

Simba Yanga WA0007 Simba Yanga; Kama vipi mmoja aongoze kundi halafu wakutane Robo Fainali

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba wana timu bora sana kuliko kipindi chote ambacho umewahi kuishuhudia Simba ikishiriki kwenye mashindano ya kimataifa, Simba ina wachezaji top kabisa na imeimprove sana.

Lakini kwa sababu na Yanga ime improve imesababisha watu wengi kutokuiangalia Simba na umahili wake.

Mechi ya juzi Simba ilikuwa na wazawa watatu kwenye kikosi cha kwanza na jana Yanga ilianza na idadi iyo iyo na wazawa watatu, Simba ilianza na Aishi, Zimbwe, Inonga na Chama wote wakiwa wametoka AFCON.

Kuna Kanoute kutoka Mali, Che Malone Cameroon, Inonga Congo mbele ni Jobe maana yangu ni kwamba Simba ina wachezaji bora.

Ukirudi kwa Yanga ilikuwa na wachezaji sita waliotoka AFCON, Diarra [Mali] Job, Bacca na Mudathir [ Tanzania], Aziz Ki [ Burkina Faso ] Musonda [Zambia] na katika magoli manne magoli matatu wamefunga wachezaji watatu waliotoka AFCON hii ni tofauti na Belouizdad ilikuwa haina mchezaji hata mmoja aliyeshiriki michuano ya Afcon.

Kuhusu Simba sasa wao wakishinda mechi yao na Jwaneng wamefuzu moja kwa moja wao wanatakiwa kushinda tu ila mimi natamani mmoja kati ya Simba au Yanga mmoja aongoze kundi ikiwezekana Robo Fainali wakutane wao kwa wao ili mmoja atumike kama ngazi ya kumpeleka mwingine Nusu Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live