Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga, Azam wakutana chanjoni Muhimbili

Muhimbili Pic Data Viongozi wa Simba

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Timu tatu za juu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga na Azam leo zilikuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya kupata chanjo ya uviko (Covid-19).

Waachezaji na viongozi wa timu zote tatu walifika Hospitalini hapo kuanzia mida ya saa tano asubuhi na kuendelea na huduma za kiafya.

Nyota wa Yanga, Tonombe Mukoko, Abdallah Shaibu na Adeyum Saleh ni miongoni mwa wachezaji waliofika Hospitalini hapo sambamba na baadhi ya viongozi wao wakiwemo, Mhandisi Hersi Said na wakili Patrick Simon.

Kwa upande wa Simba, wachezaji na viongozi wa timu ya wanawake (Simba Queens), ndio walifika mapema Muhimbili na kuendelea na taratibu za hospitalini hapo huku baadhi ya viongozi wa timu kumbwa wakionekana katika maeneo tofauti ya Hospitali hiyo na baadae nao kuendelea na taratibu sambamba na baadhi ya wachezaji.

Azam nao hawakuwa mbali kwani gari lao lilikuwa limepaki katika viunga vya hospitali hiyo ambapo wachezaji kadhaa akiwemo Nicolaus Wadada walionekana pamoja na viongozi akiwemo Ofisa Habari wa timu hiyo Zakaria Thabit, kocha mkuu George Lwandamina na wengine ambao baadae waliendelea na taratibu za kupata chanjo.

Timu zote hizo zinajiandaa na michuano ya kimataifa itakayoanza mwezi ujao ambapo Simba na Yanga zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam watakuwa katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: Mwanaspoti