Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Yafanya Umafia Niger

Simba 234 Simba Yafanya Umafia Niger

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UNAAMBIWA Simba tayari imetanguliza jeshi la siri nchini Niger kwa lengo la kuweka mambo sawa kabla ya timu kwenda kupambana na US Gendamarie ya nchini humo, wikiendi hii.

Jumapili hii, Simba inatarajiwa kupambana na US Gendarmerie ukiwa ni mchezo wa Kundi D la Kombea la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa Général Seyni Kountché uliopo Niamey, Niger.

Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa timu zote ambapo awali Simba ilishinda 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas, wakati US Gendamarie ikifungwa 5-3 na RS Berkane.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimesema kwamba, pamoja na kuwa na michezo ya ndani tayari uongozi umetanguliza mashushu wake kwenda Niger ili kuhakikisha wanasoma mazingira ya nchi hiyo.

“Tunashukuru sana uongozi kwa kupata uzoefu mkubwa katika mashindano haya ya kimataifa, maana pamoja na kuhitajika kusafiri kwa pamoja, tayari kuna jeshi la siri linatarajiwa kuingia Niger kesho (leo Alhamisi) ili kuhakikisha wanasoma ramani zote za mazingira ya nchi hiyo.

“Uongozi umefanya hivyo kutokana na kuwepo na wimbi la hujuma kwa wageni kwani katika michuano hii karibia kila timu inahitaji kuvuna pointi tatu nyumbani jambo ambalo hata sisi tunalijua, hivyo kwa kutambua hilo tumejipanga kupata ushindi ugenini au sare ndiyo maana kuna watu wanatangulia kusoma mazigira,” kilisema chanzo hicho.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Ni kweli tupo kwenye mipango ya kuhakikisha watu wanasafiri mapema iwezekanavyo kwenda Niger na kwamba mara baada ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting, mipango yote ya kikosi kuondoka itakuwa tayari na tutawafahamisha siku husika.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live