Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Week kuanzia Morogoro

Simba Day.jpeg Simba Week kuanzia Morogoro

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wametangaza rasmi kuwa Wiki ya Simba SC (Simba Day) inazinduliwa rasmi siku ya Jumatano Mkoani Morogoro.

Simba SC wataenda Morogoro wakiwa na kauli mbiu yao ya Ubaya Ubwela kwa treni ya Mwendokasi ya SGR na baada ya kumaliza kuzindua Simba Day moja kwa moja wataelekea Mikumi kwa ajili ya Uzinduzi wa jezi zao mpya za msimu wa 2024/25.

Tukio hilo la Simba SC limetangazwa na Afisa Mtendaji Mkuu wao Imani Kajula kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogoda na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mikumi Augustine Masesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live