Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Vitani Leo Kutetea Kombe la Shirikisho

Simba Waondoka Zam Simba Vitani Leo Kutetea Kombe la Shirikisho

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SIMBA ya Dar es Salaam leo saa moja usiku, inashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya JKT Tanzania.

Simba itaingia uwanjani baada ya Jumamosi kutoka 0-0 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mechi nyingine zinazotarajiwa kufanyika leo kuanzia saa 10 alasiri ni Dodoma Jiji itaikaribisha Pan African, Uwanja wa Jamhuri, Namungo F itakuwa mwenyeji wa Mashujaa Uwanja wa Ilulu, Ruvu Shooting itavaana na Gwambina Uwanja wa Mabatini Pwani na Mbeya Kwanza itakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kuivaa Mwadui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live