Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tutapitia ripoti ya Mgunda kufanya usajili mpya

Mgunda X Kibu Mgunda na Kibu.

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuwa itapitia ripoti ya Kaimu Kocha Mkuu wao, Juma Mgunda kwa ajili ya usajili mpya kuelekea msimu ujao wa Ligi.

hayo yamesemwa na Meneja Habari na Mawasilino Simba SC, Ahmed Ally ikiwa ni siku chache baada ya Mgunda kukabidhiwa timu hiyo kurithi mikoba ya kocha Abdelhak Benchikha aliyevunja mkataba.

“Uongozi utapitia ripoti ya Benchi la Ufundi lililopo chini ya Juma Mgunda pamoja na Kamati ya ufundi baada ya msimu huu kumalizika ili wajue ni sehemu gani za kupaboresha.”

“Tutafanya maamuzi magumu kwa lengo la kuiboresha timu yetu, ninaamini kila Mwanachama na Shabiki wa Simba SC atafurahi kitakachofanyika katika kipindi cha usajili wa kuelekea msimu ujao 2024/25.”

"Ninaomba Wanachama na Mashabiki wa Simba SC wasiwe na wasiwasi msimu ujao tutafanya mabadiliko ambayo yatamwacha mdomo wazi kila mtu, tumedhamiria makubwa tunataka turudishe heshima yetu ya mwanzo," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live