Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tunarudisha mataji yote

Barbara Gonzales CEO Simba Simba: Tunarudisha mataji yote

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa msimu huu klabu hiyo imejipanga kurudisha makombe yote ya ndani na kuhakikisha inafika nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Barbara ameyasema hayo jana kwenye uzinduzi wa Simba Week ulifanyika Mbagala Zakheim Dar es salaam ambapo pia ameongeza kuwa usajili bado unaendelea na kuanzia wiki ijayo wataendelea kushusha wachezaji wengine.

“Safari hii hakuna kuteleza tena. Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mataji yote kuanzia Ligi Kuu, FA na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika”

Kuelekea kilele cha Simba Day ambayo itafanyika Agosti 8, 2022 Simba imezindua Slagan Mpya We Are Unstoppable Hatushikiki Hatuzuiliki.

Msimu uliopita Simba ilizisiwa ujanja na watani zao Yanga baada ya kuzoa makombe yote ikiwemo la ligi kuu ya Nbc, pamoja na Kombe la shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) na Ngao ya Jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live