Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tunaondoka na Ngao ya Jamii kwa Mkapa

Zoran Maki 1 1140x640 Simba watamba kuondoka na Ngao ya Jamii

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba Zoran Maki ameweka wazi kuwa anaamini kwamba watapata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kutokana na maandalizi na hana hofu na mechi hiyo.

Maki ambaye ni mrithi wa mikoba ya Pablo Franco aliyefungashiwa virago Mei 31, mwaka huu, kete yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Yanga, Agosti 13 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Maki alisema kuwa anatambua kuhusu ratiba ilivyo na mechi kubwa ambazo atakutana nazo ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Yanga.

“Kikubwa ni kuheshimu kila mchezo, najua kwamba kuna Dabi hilo lipo wazi na hata ambapo nilikuwa kulikuwa na jambo kama hili hivyo sina mashaka na mchezo wetu dhidi ya Yanga kikubwa ni maandalizi mazuri.” Alisema Maki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live