Kocha wa makipa Simba, Daniel Cadena ameweka wazi juu ya mabadiliko na kutokuwa na kipa namba moja, walikuwepo ndani ya kikosi cha timu hiyo wameonyesha uwezo mkubwa kila anapopata nafasi.
Amesema katika mashindano ya kombe la Mapinduzi na michezo sita ya mwisho ya mzunguko wa kwanza makipa wote walifanikiwa kucheza na kufanya vizuri hali ambayo inakuwa ngumu kuweka kumpata kipa namba mmoja ndani ya kikosi chao.
Katika michezo sita ambayo Simba imecheza baada ya mapumziko mafupi kupisha michuano ya AFCON, tayari makipa watatu kati ya wanne wameonekana katika michezo toafuti, akiwemo Ayoub alidaka mechi tatu dhidi ya JKT Tanzania, Azam FC na Tabora United.
Kwa upande Aishi Manula amesimama katika mlingoni katika mchezo kati ya Geita Gold FC na Mashujaa FC na Hussein Abel alidaka mechi moja ya Kombe la Shirikisho FA dhidi ya Tembo FC ya Tabora, uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam.
Mocha huyo amesema kulingana na ubora wa makipa walionao wamekuwa na wakati mgumu wa kuweza kupata kipa namba mmoja na kila mtu amekuwa akipewa nafasi ya kucheza kila mechi.
Amesema anajivunia kuona makipa wake wanakuwa imara zaidi na kusaidia timu kupata matokeo chanya ikiwemo Ayoub Lakred, mechi ya juzi aliweza kuzuia mashuti mengi kutoka kwa wapinzani wao JKT Tanzania.
“Ninajivunia kuwa na makipa wazuri na wenye uwezo mkubwa, ukiangaliakiwanho cha Manula, Hussein, Ally hata Lakred wote wapo vizuri hata mmoja wapo asipokuwepo ndani ya timu kwa changamoto yoyite hatuna presha ya nani kukaa golini,” amesema Kocha huyo.