Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tumemfunga Azam kumkumbusha nafasi yake

Fredy Kanoute AAfcp6.jpeg Simba: Tumemfunga Azam kumkumbusha nafasi yake

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa walijua kama wangemfunga Azam Fc katika mchezo wa jana lakini hawakujua iwapo wangemfunga mabao mengi kiasi kile kutokana na ubora walio nao timu hiyo.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Niwaambie Azam Fc kwamba pale Mwanza walinusuriwa, la sivyo tungewagonga vizuri tu. Tukawaambia hawana timu ya kuifunga Simba, wakapiga kelee, tukaenda kwenye Kombe la Muungano tukawapiga, wakasema tukutane kwenye ligi, leo (jana) tumemfanya vibaya.

“Tumemfunga Azam kumkumbusha nafasi yake. Kuna wakati Azam anajisahau anaona kama anatumudu hivi, kuna wakati anaweza kutubahatisha lakini Azam sisi hatuwezi, hana ubora wa kutufunga tukiamua leo twendeni tukashinde.

“Azam kwa kuwa ana timu bora ajiandae na Kombe la Shirikisho, hana uwezo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, lazima tuseme ukweli. Apambane nafasi ya tatu ama ya nne huko, akienda klabu bingwa atadhalilisha taifa,” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live