Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Tumejipanga dhidi ya Singida Big Stars

Juma Mgunda Class Kocha Juma Mgunda

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa wamejiandaa kwenda kushindana na Singida Big Stars leo jumatano jioni.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa leo jumatano kwenye Uwanja wa Liti, Singida ambapo Singida Big Stars watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Kikosi cha Simba kiliondoka Dar juzi jumatatu kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo huo ambapo jana kilifanya maandalizi ya mwisho.

Mgunda alisema kuwa: “Wachezaji wote tulioondoka nao wapo fiti tayari kwa ajili ya mchezo huo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars.

“Tunajua Singida wana wachezaji wazuri na ukizingatia aina ya pia wapo kwenye Uwanja wao wa nyumbani hivyo mchezo utakuwa mgumu sana.

“Sisi tunaingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo kulingana na aina ya kikosi tunachoenda kukutana nacho.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live