Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa wekundu wa Msimbazi wana Lunyasi wanacheza mpira wa malengo, kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya.
Ahmed amesema hayo alipokuwa akijibu swali baada ya kuulizwa mechi dhidi ya Vipers, Mnyama alishinda lakini alicheza mpira mbovu, na ndipo alipokuja na majibu hayo akiuliza ‘Wao (wanaosema Simba mbovu) wanaangalia mpira wapi?’
“Mashindano ya klabu bingwa zilianza timu nyingi sana lakini sasa zimebaki timu 16 tu na sisi tupo, hao wengine walishatolewa kwahiyo hii inamaanisha ni Simba ni kubwa”
“Hao wenzetu wanaangalia mpira wapi, kama takwimu zinaandikwa na CAF wenyewe, mechi ya Vipers tulipiga mashuti mengi na ufanisi wa pasi ni asilimia 63, umiliki wa mpira 63 timu mbovu haiwezi kuwa hivyo”
Simba anatarajia kucheza mechi yao muhimu zaidi ya kuamua kama watasonga robo fainali au safari yao itaishia hapo, ni dhidi ya ya Horoya kwenye dimba la Mkapa siku ya Jumamosi Machi 18.