Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Singida kundi moja Mapinduzi Cup

Simba Vs Singida Chama.jpeg Simba, Singida kundi moja Mapinduzi Cup

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi wa pili kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup msimu uliopita Singida Big Stars imepangwa kundi moja na Simba kwenye mashindano hayo yanayotarajia kuanza Desemba 28 hadi Januari 13, 2024.

Singida ambayo iliyo kundi B kati ya makundi matatu yaliyopangwa yakiwa na timu nne kila moja, ipo pamoja na Jamhuri SC, APR ya Rwanda na Simba.

Yanga ipo kundi C sambamba na Bandari FC, Vital'O ya Burundi na KVZ, huku Kundi A likiwa na Mlandege FC, Azam FC, Chipukizi na URA ya Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Suleiman Mahmoud Jabir, kuhusu mashindano hayo amesema hii itakuwa ni moja kati ya michuano mikubwa na bora kushuhudiwa kutokana na aina ya timu zitakazoshiriki.

"Tunatarajia kuwa na michuano bora msimu huu kwa sababu kwanza tumeongeza timu, pia tumealika timu zenye ushindani kutoka nje," amesema.

Aidha alibainisha mechi zote katika michuano ya msimu huu zitachezwa katika Uwanja wa Amani visiwani humo. Michuano ya Mapinduzi msimu huu itakuwa ni sehemu ya shamrashamra ya kusherehekea miaka 60 tangu Mapinduzi ya Zanzibar.

Msimu uliopita, Mlandege ilivunja mwiko kwa timu za Zanzibar kutofanya vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kuibuka na taji kwa kuifunga Singida FG katika mchezo wa fainali uliochezwa Januari 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live