Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Singida FG nusu fainali ya kisasi

Simba Kukila Kiporo Chake Na Mashujaa Simba, Singida FG nusu fainali ya kisasi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imeendelea kuweka salama malengo yao ya kuchukua taji la pili msimu huu  ikitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba kwa bao 1-0.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Simba kuifuata Singida Fountain Gate ambao mapema jioni ilitangulia nusu fainali baada ya kuichapa Azam FC kwa mabao 2-1. Jamhuri ilikaza.

Simba haikuwa na dakika 90 rahisi mbele ya Jamhuri kama ambavyo ilikuwa ikidhaniwa kwani vijana hao wa Pemba walikuja na akili tofauti na mbinu na kuwabana vizuri wekundu hao kwa muda mwingi wa mchezo huo.

Jamhuri waliwabana Simba kwa kuwa bora katika njia za kupitisha mipira ya kutengeneza mashambulizi ya wekundu hao na kuwaweka kwenye presha kubwa wapinzani wao.

Simba kutumia nafasi bado

Simba ingeweza kutengeneza ushindi mzuri pengine zaidi kama washambuliaji wake Jean Baleke na Luis Miquissone wangetulia kutumia nafasi hasa kupitia krosi za mabeki wao wa pembeni wakiongozwa na Shomari Kapombe.

Jamhuri hawana watu mbele Shambulizi kali la Jamhuri lilifanyika dakika ya 83 walipofika vizuri na kupiga shuti kali ambalo hata hivyo lilipanguliwa na kipa Ayoiub Lakred  kisha kuudaka tena.

Muda mrefu ukuta wa Simba ulikuwa kwenye utulivu mkubwa kutokana na kukosa changamoto kutoka kwa washambuliaji wa Jamhuri ambao walidhibitika kirahisi.

Baleke kosa moja tu Ukuta wa Jamhuri ulifanya kosa moja tu lililowagharimu kwa kumruhusu mshambuliaji Jean Baleke kuruka juu bila kusumbuliwa na kufunga bao hilo pekee lililoamua mchezo huo akitumia krosi ya Miquissone dakika ya 45+2.

Ngoma na tuzo za mchezaji Bora Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma ni kama ameziteka tuzo za mchezaji bora za timu hiyo akichukua tuzo ya pili kwenye mechi za Singida Fountain Gate na leo dhidi ya Jamhuri.

Singida vs Simba ni kisasi Simba kwenda kukutana na Singida ni kama mechi ya kisasi kwani timu hizo zilikutana hatua ya makundi na Singida kukubali kipigo cha mabao 2-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live