Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Sc yapigwa na Al Hilal

SIMBA AL HILA 01.jfif Simba yapigwa na Al Hilal

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika, Simba Sc wameambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Al- Hilal ya Sudan katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa nchini Sudan jana usiku.

Bao hilo la Al Hilal limefungwa na John Mano kunako dakika ya 82 kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi kutoka upande wa kushoto huku akiwaacha mabeki wa Simba wakishangaa kilichotokea.

Hiyo ni mechi ya pili kwa Simba baada ya kuwafunga Asante Kotoko kutoka Ghana 4-2 wakiwa huko huko Sudan

Waliofunga magoli ya Simba katika mechi ya Asante Kotoko walikuwa ni viungo, Mghana Augustine Okrah na Osman Sakho kutoka Senegal na Mzambia Clatous Chama aliyetupia mawili.

Katika mechi hizo za mashindano ya kirafiki ya Al Hilal Super Sports ambazo zimefikia tamati, Al- Hilal ndio timu ambayo haijapoteza. Katika mechi ya kwanza, mabingwa hao wa Sudan waliwafunga Asante Kotoko 5-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live