Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Sc yafafanua dili la Bwalya kuelekea Amazulu

Bwalya Simba Rally Bwalya

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba mchezaji wake raia wa Zambia, Rally y Bwalya aanatakiwa na Klabu ya Amazulu ya nchini Qfrika Kusini.

"Iyo taarifa kama klabu haijatufikia na hata mchezaji mwenyewe amerejea juzi kutoka Zambia alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa na tukamuuliza kwamba kuna moja mbili tatu kutoka Amazulu na yeye akasema hana hizo taarifa"

"Kwahiyo tunawasubiri kama kweli ofa itakuja. Tutaangalia maslahi ya klabu na maslahi ya mchezaji tutafanya maamuzi. Na hilo tuliweke very clear, kama ofa inakuja ni nzuri hakuna namna ya kuendelea kumkeep mchezaji"

"Maisha ya klabu ni kununua wachezaji wazuri na kuuza wachezaji wazuri, huwezi kubaki na mchezaji kama umemzaa wewe mpira wa hivyo haupo. Mpira ni biashara na biashara kubwa ni kuuza na kununua wachezaji" amesema Meneja wa Mawasiliano wa @simbasctanzania - @ahmedally_ kuhusu @iamrallybwalya kwenda @amazulu_fc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live