Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Sc imemfanya Yanga kama chambo

Simba Ticket Sold Simba Sc imemfanya Yanga kama chambo

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sitaki kukuchosha nitaandika kwa ufupi katika lugha rahisi ambayo utaelewa.

Ushindani wa Vilabu vya Simba na Yanga katika nyanja zote umekuwa na faida kubwa kwa vilabu hivyo na hasara ndogo.

Hivi karibuni, ukitoa ushindani wa ndani ya pitch ambao Yanga wanaonekana kushinda lakini ushindani wa nje ya uwanja, Simba SC amegundua njia ya kushinda.

Katika matukio mbalimbali Simba SC imekuwa ikimtumia Yanga kama kioo, kutazama wapi kakwama ili yeye atatue tatizo na kulifanya jambo hilo vizuri zaidi.

◉ Katika suala la utambulisho wa jezi

◉ Katika suala utangazaji wa Bajeti.

◉ Katika suala la kujaza watu uwanjani kwenye tamasha.

Katika matukio hayo na mengine Simba SC amekuwa smart, amekuwa akimvizia Yanga kwa kumuacha afanye kwanza jambo lake aone mapungufu ili yeye aboreshe zaidi kitu ambacho sio kibaya, ni strategic plan.

Msimu huu Yanga walikuja na staili tofauti ya uzinduzi, wakazindulia jezi zao Ikulu. Simba SC baadae nae akaja na kibegi katika mlima Kilimanjaro.

◉ Yanga walitangaza kwenye mkutano mkuu kuwa Bajeti yao ya msimu ni Tsh 20 Billion. Kisha Simba SC akaja na Bajeti ya Tsh 23 Bilioni. Hata kuhusu pre-season alianza kutangaza Yanga kisha Simba akafuata.

◉ Ile hali ya kutojaza full-house kwenye Kilele cha wiki ya Mwananchi wengine wakisema ni kutokana na bei kubwa ya kiingilio, kwa upande wa Simba SC ilikuwa ni PROMOTION tosha kabisa hata kama Alikiba asingejiunga Simba au Ahmed asingepita na Kispika mtaani unajua kwa nini?

Ni kutokana na ushindani baina ya timu hizi mbili ambazo kwao kila siku ni derby, ilikuwa lazima mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi ili kuwaonesha Yanga kuwa tumewashinda kujaza uwanja.

Yanga wakikubali kuendelea kutumika kama ramani ya vita kwenye matukio mbalimbali kila msimu wataendelea kuzidiwa kete.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live