Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Sc hawana msanii mkubwa - Ngereza

Alikiba Mnyama Simba Sc hawana msanii mkubwa - Ngereza

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Alex Ngereza amesema kuwa klabu ya Simba haina msanii mkubwa ambaye ni shabiki wa timu hiyo.

Ngereza amesema hayo mara baada ya msanii ALikiba kutangaza kuhamia Simba na kuachia ngoma mpya iitwayo Mnyama huku akipewa dili la kutumbuiza kwenye Tamasha la SImba Day, Jumapili ijyo katika Uwanja wa Mkapa.

"Klabu ya Simba hawana msanii mkubwa ambaye ni shabiki wa timu yao wa kutupwa, ndiyo maana tunaona wanabadilisha wasanii wa kutumbuiza kwenye Tamasha lao kila mwaka.

"Kitu ambacho nawapongeza Simba ni kugeuza tamasha kuwa biashara wanafikiria zaidi kuwafurahisha mashabiki bila kujali kwamba wanapata burudani kutoka kwa msanii ambaye ni shabiki asilia wa timu yao au sio shabiki asilia.

"Hiki ndio kitu ambacho wanakifanya Simba ingawa Alikiba sio shabiki wa Simba lakini wameamua kumtumia kibiashara zaidi, sisi tunafahamu kwamba shabiki halisi wa Simba SC ni Diamond Plutnumz." amesema Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live