Klabu ya Simba imesema kuwa, sasa ni wakati wa kumvua taji bingwa mtetezi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika wa msimu uliopita, Wydad Casablanca ya Misri.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally mara baada ya Simba kupangwa kucheza na Wydad katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo.
“Ni lazima tukiri kuwa tumepata mpinzani mgumu kwenye hatua ya Robo Fainali na pengine ni mpinzani mgumu zaidi tangu tuanze kushiriki hatua hii.
"Hapa unamzungumzia bingwa mtetezi, unamzungumzia mshiriki wa Club world Cup, unazungumzia timu yenye wachezaji waliotoka nusu fainali ya kombe.
"Huu ni mlima mrefu kwetu lakini hatuna budi kuupanda na kufika kileleni. Ili uwe mkubwa Afrika ni lazima uwafunge wakubwa wa bara hili.
"Inawezekana sana Simba kupata ushindi dhidi ya Wydad kama tuu kila idara ndani ya taasisi yetu itatimiza wajibu wake kwa asilimia 100 Kama tulivyomvua Ubingwa Zamalek mwaka 2003 ni wakati sasa kumvua Ubingwa Wydad,” amesema Wydad.