Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Safari hii litakufa jitu fedha tunazo

HAJI MANARA AHMED Ahmed Ally na Haji Manara

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmedy Ally, amesema Rais wa heshima wa klabu hiyo Mo Dewj, ametenga fedha za kusajili kila mchezaji atakayehitajika katika klabu hiyo.

Ahmedy amesema juzi Juni 11, wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Simba Kisukuru lililopo Tabata, jijini Dar Es Salaamu.

"Kila ambae atasajiliwa atawekwa hadharani wana Simba mtaonyeshwa, wana Simba mtaambiwa.

"Niwaambie tu kwamba safari hii litakufa jitu, tunafanya usajili wa maana sana kwasababu fedha ipo.

"Rais wa heshima, Mohammed dewj ametenga fedha ya kutosha ya kuweza kusajili kila mchezaji ambae tunamhitaji, na hatimae anatua Simba Sc.

"Ukiona tumeacha kumsajili mchezaji pamoja na kwamba ni mzuri lakini jua kwamba fedha walioitaka haifanani na thamani ya ya huyo mchezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live