Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC yakomaa na CAF Super League

Simba Warejea Mazoezini Kuwawinda Polisi, Coastal Simba SC yakomaa na CAF Super League

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya jambo ambalo Simba SC wamejadili ni usajili kwa ajili ya michuano mipya ya Super Cup, lakini pia maandalizi ya kambi yao ya kabla ya msimu ujao kuanza.

Chanzo cha ndani kutoka ndani ya kikao hicho kinasema kuwa mabosi walibishana kuhusu aina ya usajili waliokuwa wakifanya, huku wakihusisha na vigogo kadhaa ambao watapambana nao kwenye Super Cup, kama Mamelodi Sundowns, Al Ahly na hata Wydad Casablanca.

"Tulijadili mambo mengi, lakini kubwa ni usajili kwa ajili ya mashindano ya Super Cup yanayoanza mwezi Agosti, hapa tulijadili mambo mengi lakini ugumu pia wa ratiba.

"Wajumbe walikuwa wakali kwa kuwa wanaamini mashindano haya ndiyo yataonyesha tuna kikosi cha namna gani kwa kuwa tunakwenda kupambana na vigogo wa Afrika, huku hakuna timu ndogo ndiyo maana unaona tumekaa muda mrefu," alisema bosi huyo na kuongeza:

"Hata hivyo, ishu ya kambi naona tuliimaliza kwa kuwa wengi walipendekeza timu iende Uturuki baadaye mwezi ujao, bado tutalijadili lakini hili limeshapita labda kuwe na ishu nyingine."

Chanzo hicho kilisema majina kadhaa yametajwa kwenye usajili, lakini utaratibu maalumu wa kuwatangaza umeshawekwa sawa.

"Kuna wachezaji nafikiri ni watatu tayari tumeshawasajili, klabu inasubiri dirisha lifunguliwe ndiyo watangazwe rasmi kuna utaratibu umewekwa, wengine tunaendelea kubishana ili kuhakikisha tunapata wale bora kwa kuwa fedha za Super Cup zipo hivyo hakuna shida sana," kimesema chanzo.

Timu nane zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Super Cup ambayo ni mapya na yatachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini ambazo ni Petro de Luanda (Angola), Mazembe (DR Congo), Mamelodi (Afrika Kusini) Horoya (Guinea), Wydad Atheltic Club (Morocco), Al Ahly (Misri) Simba SC (Tanzania) na Esperance de Tunis (Tunisia).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: