Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC yaichakaza Mtibwa Sugar, Azam, Namungo hazikamatiki

95383 Pic+matokeoo Simba SC yaichakaza Mtibwa Sugar, Azam, Namungo hazikamatiki

Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imeendelea kujikita kileleni baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Katika mchezo huo Simba ilipata mabao yake kupitia nahodha John Bocco, beki Mohamed Hussein na kiungo Hassan Dilunga. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 53, kifuatiwa na Azam (44) Yanga (37) kabla ya mechi yake dhidi ya Mbao na Namungo ikiwa ya nne na pointi 36. Katika mchezo huo Simba ikiwa na msuguano ya chinichini tangu ilipochwa na JKT Tanzania ilicheza kwa kujiamini zaidi na kuwapa wakati mgumu Mtibwa Sugar. Mtibwa Sugar iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Simba katika fainali iliyofanyika Zanzibar ilionekana kupoteza ubora wa uchezaji. Wakati mchezo huo ukiwa unaelekea mwishoni mwa kipindi cha kwanza dakika 45+1, nahodha Bocco alipokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere aliwazidi ujanja mabeki wa Mtibwa kwa kuugonga mpira uliokwenda pembeni na kutumbukia wavuni. Bao hilo lilifanya Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0, waliporudi kipindi cha pili walikuja kwa kasi zaidi. Beki Hussein Zimbwe JR alifunga bao pili katika dakika 47, akipiga krosi iliyokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kardo akiruka bila ya mafanikio. Simba ilihitimisha kalamu yake ya ushindi katika dakika 59, wakati kiungo Dilunga alipotumia vizuri pasi ya Francis Kahata na kupiga shuti la chini lililojaa wavuni. Akizungumzia mchezo huo kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amesifu wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kupata ushindi huo. “Wachezaji wangu wamecheza vizuri na kujituma vizuri muda wote jambo lililosaidia kupata ushindi huo muhimu baada ya kupoteza mechi iliyopita,” alisema Sven. Azam, Ndanda, Namungo, Biashara United zagawa dozi Bao la kiungo Mudathir Yahya limetosha kuipa Azam ushindi bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mudathir alifunga bao hilo pekee kwa shuti kali katika dakika 48, lililomshinda kipa wa Polisi Tanzania, Mohamed Ally na kujaa wavuni. Matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 44 itaendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hata kama Yanga baadae itashinda dhidi ya Mbeya City haitaweza kuzifikia pointi za Azam FC. Katika michezo mingine, Biashara United ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC shukrani kwa bao la Atupele Green katika dakika 63. Ndanda imeendeleza rekodi yake ya ushindi baada ya kuichapa Mwadui Fc kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. Katika mchezo huo mabao ya Ndanda yalifungwa na Samwel John katika dakika 69, na Ommary Khamis (89). Kagera Sugar ikiwa nyumbani Kaitaba ilikubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Alliance, Safari ya Singida United kushuka daraja imezidi kushika kasi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Namungo kwenye Uwanja wa Namfua, Singida. Lipuli ikiwa nyumbani imelazimishwa sare 1-1 na JKT Tanzania. MECHI IMEAHIRISHWA Mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Tanzania Prisons uliokuwa uchezwe kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani umeahirishwa baada ya gari ya huduma ya kwanza (Ambulance) kuchelewa kufika uwanjani hapo.

Chanzo: mwananchi.co.tz