Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC wapewe maua yao

Simbasctanzania 1695805638773.jpeg Simba Sc

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ninaamini timu ya Simba SC wanapaswa kupewa hongera nyingi sana kwa kutuletea African Footbal League (AFL) nchini Tanzania.

Hakika hii ni fursa nzuri na kubwa kwa taifa letu kwani timu ya Simba SC imeleta neema kwa timu zingine na wachezaji wetu pia.

dunia ya mpira imetujua zaidi. Ahsante Simba SC kwa kutuletea wageni wa zito kutoka ulaya na afrika kwa ujumla.

Ujio wa raisi wa FIFA duniani, ujio wa raisi wa CAF Africa na ujio wa Kocha maarufu duniani Arsene Wenger hakika hii ni heshima kubwa kwa taifa letu.

Hawa wote na wengineo wataingia ndani ya Benjamin Mkapa Stadium, hii ni heshima kubwa kwa Uwanja wetu na ardhi yetu.

Pia mechi itarushwa dunia nzima kupitia channel kubwa duniani FIFA TV. Hakika jina la Tanzania na Simba SC vimetrend duniani na hii ni baraka kwetu.

Haya yote yanatokana na Simba SC kufanya vizuri kimataifa na kujikusanyia points nzuri ambazo zimewaweka sehemu nzuri.

Hongera Simba SC Hongera Tanzania Hongera TFF Hongera CAF Hongera FIFA

Kizuri kipewe sifa zinazostahili, hakika Simba SC wamejua kutuheshimisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live