Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC wametua salama Niger, tayari kwa mchezo

Simba Niger wachezaji wa Simba wakiwa uwanja wa ndege nchini Niger

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Kikosi cha Simba SC kimefika salama nchini Niger jana jioni tayari kwa mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao US Gendarmerie. Timu hizi mbili zitashuka dimbani kesho kuwania alama 3 katika muendelezo wa michezo ya hatua ya makundi.

Kikosi cha Simba SC kiliondoka jijini Dar es salaam juzi majira ya Saa 11 jioni kikiwa na wachezaji 23 pamoja na viongozi. Mchezo huu utachezwa le majira ya Saa 1:00 Usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania katika uwanja wa Stade Général Seyni Kountché uliopo mji mkuu wa Niger Niamey.

Mchezo huu ni wa pili kwenye michezo ya hatua ya makundi na timu hizi zimepangwa Kundi D, Mchezo wa kwanza Simba iliifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast mabao 3-0 wakati Gendarmeri wao walifungwa ugenini na RS Berkane mabao 5-3.

Chanzo: eatv.tv