Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC waitisha Mkutano Mkuu

Simba SC Waitisha Mkutano Mkuu Simba SC waitisha Mkutano Mkuu

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club imewataarifu wanachama wake kuwa Mkutano Mkuu wa Mwaka utafanyika Jumapili Desemba 21, 2023 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Centre (JNICC).

Kwa mujibu wa barua waliyoichapisha kwenye ukurasa wao wa Instagram, ajenda za Mkutano huo zimeainishwa katika ibara ya 22 ya Katiba ya Simba Sports Club, 218. Taarifa hiyo imeeleza pia kufuatia maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), moja wapo wa ajenda itakayojadiliwa ni mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Simba SC hivyo Bodi imeunda Kamati Maalum ya kuratibu mchakato wa Marekebisho ya Katiba.

Wajumbe hao ni Wakili Hussein Kitta Mlinga (Mwenyekiti), Wakili Aziza Omary (Makamu Mwenyekiti), Ustadhi Masoud (mjumbe), Zulfika Chandoo (mjumbe), Wakili Moses Stewart Kaluwa (mjumbe), Hamis Mkomwa (mjumbe) na Mohamed Khamis Soloka (mjumbe).

Bodi imewaalika wanachama wenye mapendekezo ya marekebisho ya katiba wayawasilishe katika ofisi za Sekretarieti au kupitia barua pepe ya simbasc.co.tz kabla ya Desemba 30, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live