Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC majaribio kwa Yanga Septemba 25

SIMBA TRAIN ARUSHA Kikosi cha Simba kikijifua Arusha

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umeweka wazi kwamba hesabu zao kwa msimu wa 2021/22 ni kukusanya kila taji ambalo Simba itashiriki na tayari wanajua sehemu ya kuanzia ni mbele ya Yanga, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes msimu uliopita kilitwaa taji la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na kilinyanyua pia na Ngao ya Jamii mbele ya Namungo, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa tayari mipango imekaa sawa na wanajua sehemu ya kuanzia itakuwa wapi kuchukua mataji yao waliyotwaa msimu uliopita.

“Timu ni lazima iwe na mipango na mikakati, kwetu sisi tunaanza na mchezo wetu wa Septemba 25, (dhidi ya Yanga), baada ya hapo tukimaliza itakuwa ni kwenye ligi,Kombe la Shirikisho.

“Pia tunajua kwamba tunashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na huko pia kimataifa lazima tufanye vizuri, jambo la msingi ni mashabiki kuwa bega kwa bega na sisi na tunashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa nasi,” amesema.

Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi Jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 na Septemba 19 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya TP Mazembe kwenye maadhimisho ya Tamasha la Simba Day.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live