Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC kuandika rekodi Ivory Coast

Ahmed Ally Awatetea Mastraika Simba .jpeg Simba SC kufumua rekodi Abidjan

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola ametamba kuwa wamekwenda nchini Ivory Coast kwa kazi mbili, kushinda mechi ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini pia kutibua Rekodi ya wapinzani wao ambao hawajapoteza mechi yoyote kwenye Kundi B.

Simba SC iliwasili Abidjan-Ivory Coast jana jioni kwa saa za nchini humo ikiwa na lengo la kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo huo, na moja kati ya walichokiangalia ni kutoruhusu bao katika mchezo huo utakaochezwa uwanja wa uwanja wa Felix, Houphouel- Boign, keshokutwa Ijumaa (Februari 23).

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema Benchi la Ufundi na wachezaji wanatambua ugumu wa mechi hiyo na wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kupambania timu kupata matokeo chanya.

Amesema ugumu wa Asec Mimosas ni kupata Rekodi nzuri katika michuano hiyo kwa kuongoza kundi hilo lakini wamejiandaa kutibua rekodi hiyo kwa kutoruhusu kufungwa katika mchezo huo na kutumia nafasi zinazopatikana.

“Tumewaangalia Asec Mimosas hivi karibuni tunaenda kucheza na timu ngumu, kuendeleza rekodi yake lakini kwa upande wetu tumejipanga vizuri safu ya ulinzi kuwa makini na washambulia wa wapinzani na washambuliaji wetu kupewa majukumu ya kuhakikisha tunavuna alama muhimu katika mchezo wetu.

Kurejea kwa beki wetu, Henock Inonga ni jambo zuri kwa sababu anazidi kuimarisha safu ya ulinzi kwa kutibua mipango yao na kupambana kutafuta pointi ugenini na kuja kushinda katika mechi yetu ya nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy ,” amesema Matola.

Ameongeza kuwa wakifanikiwa kupata alama Asec Mimosas na kushinda mechi yao ya nyumabini, watafikia malengo yao ya kufuzu na kwenda kucheza Robo Fainali ya michuano hiyo.

Kuhusu kukosekana kwa Mlinda Lango kutoka nchini Morocco Ayoub Lakred kutokana na kutumia adhabu ya kadi tatu za njano, Matola amesema hawana Presha sana juu ya kumkosa nyanda huyo kwa sababu katika nafasi hiyo ina watu na kuweza kufanya vizuri.

Katika msimamo wa Kundi B, Asec Mimosas anaongoza akiwa na alama 10, Simba SC ikishika nafasi ya pili kwa alama 5, Jwaneng Galaxy wana alama 4 na Wydad Casablanca wakishika mkia katika Kundi hilo wakikusanya alama tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live