Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens yaua, Alliance yaweka heshima Nyamagana

Queens Pic Wachezaji wa Simba Queens

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu za Simba Queens ya jijini Dar es Salaam na Alliance Girls ya Mwanza zimeanza kwa ushindi katika michezo yao ya kwanza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL) iliyofunguliwa leo Desemba 23.

Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Simba Queens wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Mo Simba Arena wameishushia kipigo cha aina yake cha mabao 15-0 Ruvuma Queens.

Katika mchezo huo mastaa wa Simba Queens Oppa Clement Zena Khamis, Jackline Albert na Asha Jafari walifunga mabao hat-trickĀ  kila mmoja.

Zena Khamis alifunga mnamo dakika ya 13, 25 na 45, Oppa Clement akifunga dakika ya 36, 81 na 87, Asha Jafari akiweka kambani mnamo dakika ya 17, 32 na 40 huku Jackline Albert akifunga dakika ya 44, 51 na 90.

Mabao mengine yalifungwa na Aisha Juma (73) huku mawili wachezaji wa Ruvuma Queens wakijifunga.

Wachezaji wa Alliance Girls wakishangilia ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Mlandizi Queens leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Katika mchezo mwingine uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza wenyeji Alliance Girls wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mlandizi Queens ya Pwani.

Alliance walipata bao hilo mnamo dakika ya 78 likifungwa na Winfrida Charles baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Mlandizi na kutandika shuti kali lililomshinda kipa Niwael Khalfani.

Kocha wa Alliance Girls, Sultan Juma amewapongeza wachezaji na kuomba muda wa kuendelea kuiboresha timu hiyo baada ya kubeba mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ezekiel chobanka aliyetimikia The Tigers ya Arusha.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz