Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens yatepeta kwa Lady doves

KICHAPO SIQUEE Mchezaji wa Simba Queens akipiga shuti mbele ya walinzi wa Lady Doves

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la CECAFA kwa upande wa wanawake yanayoendelea nchini Kenya, Timu ya Simba Queens hatimaye imekamilisha mchezo wake wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Lady Doves ya Uganda.

Timu ya Simba Queens imepokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Lady Doves ya Uganda katika mechi ya kumsaka mshindi wa tatu wa Michuano hiyo.

Timu ya Lady Doves na Simba Queens leo zimekutana kwa mara ya pili ndani ya michuano hii ya CAF Womens Champions League 2021 Qualifiers kwani walikua wote pamoja katika Kundi A.

Katika mchezo wa Kwanza wa Makundi timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, lakini leo Wakali hao kutoka Uganda wamewapa somo Simba Queens.

Fainali ya Mashindano hayo itapigwa Septemba 9, kati ya Vihiga Queens kutoka Kenya dhidi ya Commercial Bank of Ethiopia (CBE).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live