Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens yamaliza nafasi ya nne, yaacha rekodi hii

C9FCCB69 6E3E 4BF0 B54C FC8315AB9407.jpeg Simba Queens imeshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba Queens jana ilimaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Wanawake Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Bayelsa Queens ya Nigeria bao pelee la mshambuliaji Juliet Chinonso Uwanja wa Prince Moulay El Hassan Jijini Rabat nchini Morocco.

Kwa kushika nafasi ya nne Simba Queens itazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 200,000 sawa na Bayelsa Queens kama wana Nusu Fainali, wakati bingwa atapata dola 400,000 na mshindi wa pili dola 250,000.

Timu mbili zilizomaliza nafasi ya tatu katika makundi dola 150,000 kila moja na nyingine mbili zilizoshika mkia dola 100,000 kila moja.

Simba Queens imeshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza na imefanikiwa kufanya vyema katika michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live