Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens yajivunia Kikosi

Simba Queens Tz 00 Simba Queens

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula, amedai kitendo cha kubadilisha  kikosi katika kila mechi kimemsaidia kufahamu uwezo wa kila mchezaji na sasa anaweza kupata matokeo mazuri kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza.

Simba Queens iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Ceasiaa Queens, shukrani kwa Vivian Corazone aliyefunga magoli mawili pamoja na Aisha Juma na Asha Djafa.

Katika mchezo wa juzi safu ya ulinzi ilikuwa na mabadiliko kidogo kwa kucheza Daniela Ngoyi, Fatuma Issa (Fetty Densa) safu ya ushambuliaji akicheza Asha Juma, mechi iliyopita na Baobab Queens walicheza Esther Mayala, Doto Evarist na Oppa Clement.

Lukula alisema kila mechi amekuwa akifanya mabadiliko ya kikosi kwa sababu anahitajika kutoa nafasi kwa kila mchezaji ili kuisaidia timu.

Kocha huyo alisema baada ya kumkosa mshambuliaji wao, Oppa Clement, alimpa nafasi Asha (Juma) ambaye naye alifanya vizuri majukumu yake.

Aliongeza ligi hiyo imekuwa na ushindani mkubwa na mabadiliko hayo yanamsaidia kuimarisha kikosi chake na wanatambua kila mechi kwao ni fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live