Simba Queens wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Wanawake Serengeti Lite Wwomen's Premier League baada ya jana Februari 14, 2023 kuibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Ceasiaa Queens mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Aliyeanza kuandika akaunti ya magoli katika mchezo huo ni Kiungo Vivian Corazone aliyetupia shuti kali nje ya 18 dakika ya 42 baada ya kupokea pasi ya kutengewa na Pambani Kuzoya.
Kipindi cha pili Simba Queens walirejea kwa kasi na kulishambulia lango la wapinzani wao hao ambapo dakika ya 67. Asha Mnuka alipata bao la pili kisha Asha Djafar naye akapiga chuma nyingine dakika nne baadaye.
Baadaye Asha alirejea tena kambani na kukamilisha ushindi huo wa 4-0. Kwa ushindi huo Simba wamejikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ya wanawake wakiwa na alama 22 baada ya kucheza michezo tisa.
Wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo ni JKT Queens ambao wana pointi 18 wakiwa wamecheza michezo nane huku Yanga Princess wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17 katika michezo yao nane waliyocheza.