Timu ya wanawake ya Simba Queens, wametamba kuwa watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanamfunga mtani wao Yanga Princess katika mchezo huo wa dabi utakaopigwa kesho Marchi 22, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari, Kocha wa Simba Queens, Charles Lukula, amesema, mchezo wa kesho wanauchukulia kwa uzito mkubwa kwani ndoto zao ni kushinda Ligi Kuu kisha CECAFA na baadaye Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Tunaenda kesho kucheza derby tukiwa tunaongoza hatutaki kupoteza alama yoyote kwa kuwa lengo letu ni kuchukua ubingwa ili tupate nafasi ya kushiriki CECAFA na baadaye Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Lukula.