Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens na dakika 90 za maajabu, historia

Simba Queens Qq Wachezaji wa Simba Queens wana nafasi ya kuweka rekodi mpya leo

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba Queens wanatarajia kushuka dimbani kesho Jumatano kucheza mechi ya nusu fainali na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita Mamelody Sundowns kutoka Kanda ya Cosafa na Afrika Kusini.

Simba watashuka dimbani kucheza mchezo huo kwenye mji wa Rabat saa 11 jioni ikiwa ni mara ya kwanza wanafika kwenye hatua hiyo. Simba walikusanya alama sita kwenye kundi A nyuma ya AS Far.

Mchezo mwingine wa nusu fainali hiyo ni kati ya majirani wa Tanzania TP Mazembe kutoka DR Congo, ambao watacheza na AS Far saa 4 usiku wa leo.

Kocha wa Simba, Charles Alex Lukula alisema kuwa: “Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo, ingawaje kila mmoja wetu anajua kuwa tunakwenda kukutana na timu bora na bingwa wa mashindano haya.

“Tutajitolea kwa kila namna sisi kama makocha kuhakikisha tunawakumbusha vijana kuwa umuhimu wa kushinda mechi hii ni mkubwa sana.”

Opah Clemant, nahodha wa timu hiyo amesema kuwa: “Sisi tupo tayari kwa mchezo huo ambao unakwenda kuwa mgumu. Tupo tayari kwa kila kitu na ninaimani tunakwenda kushinda.”

Simba hawana cha kupoteza kwenye mchezo huo kwa kuwa wameshafikia kwenye malengo waliyojiwekea ya kutinga kwenye nusu fainali na wanacheza mchezo huo kama ni zaidi ya matarajio waliyofikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live