Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens moto wao usipime Afrika

Simba Queens Wc Simba Queens moto wao usipime Afrika

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, wawakilishi pekee wa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Simba Queens itakutana na bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Mamelodi Sundowns Womens ya Afrika Kusini leo Jumatano huku Wekundu wakitamba kutwaa ubingwa huo.

Akizungumza Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula aliweka wazi shauku yake ya kutaka kutinga fainali na kuchukua ubingwa huo.

“Kila timu imejipanga vizuri, tutacheza na Mamelodi, moja ya timu imara na zenye uzoefu wa kutosha lakini tunaendelea kujipanga ili tufanye vizuri na kutinga fainali,” alisema Lukula.

Simba ilikuwa Kundi A sambamba na timu za Determine Girls ya Liberia, Green Buffaloes ya Zambia na wenyeji AS FAR ya Morocco na kucheza mechi tatu ikishinda mbili, ikipoteza moja mbele ya AS FAR ilipofungwa mabao 2-1.

Ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya Buffalloes uliifanya Simba kushika nafasi ya pili kwenye kundi hilo na ikizoa alama sita na kuungana na AS FAR ikiwana alama tisa na kutinga nusu fainali.

Wakati Wana Msimbazi wakifurahia rekodi na kiasi cha fedha Dola 200,000 (Sh 466 milioni), ambazo ni zawadi ya kufika hatua hiyo, juzi wamemjua mpinzani wao watakayekutana naye nusu fainali kuwa ni Mamelodi Sundowns walioichakaza TP Mazembe ya DR Congo mabao 4-0 kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B.

Mamelodi ilikuwa Kundi B pamoja na Bayelsa ya Niger, TP Mazembe na Wadi Degla ya Misri na kushinda mechi zote tatu ikiongoza kundi na kutinga nusu fainali sambamba na Bayelsa huku Mazembe na Wadi Degla zikitupwa nje.

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kushiriki mashindano hayo ikiwa ni msimu wake wa pili huku mpinzani wao, Mamelodi akishiriki kwa mara ya pili baada ya kubeba ubingwa mwaka jana nchini Misri.

Chanzo: Mwanaspoti