Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens mguu sawa Afrika

Simba Queens TZC Simba Queens mguu sawa Afrika

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Simba Queens itaanza harakati zake za kuutafuta ubingwa wa Afrika kwa kuwavaa wenyeji, ASFAR FC katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Oktoba 30 kwenye Uwanja wa Prince Heritier Moulay nchini Morocco.

Mashindano hayo yatakayoanza Oktoba 30 hadi Novemba 13 yanashirikisha timu nane ambapo kutoka kundi A ni Simba Queens (Tanzania), ASFAR FC (Morocco), Green Buffaloes (Zambia) na Determine Girls ya Liberia wakati kundi B lina timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Bayelsa Queens (Nigeria), Wadi Degla FC (Misri) na TP Mazembe ya DR Congo.

Baada ya mchezo huo dhidi ya wenyeji, Simba Queens itashuka tena uwanjani Novemba 2 kwa kuikabili Determine Girls kwenye uwanja huo huo na itamaliza hatua ya makundi kwa kucheza na Green Buffaloes FC Nov. 5 kwenye Uwanja wa Grand Stade De Marrakech.

Simba Queens ilifuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa kanda ya CECAFA kwa kuifunga She Corporates ya Uganda bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali. Mabingwa hao wa Ligi Kuu bara ya wanawake hivi sasa wako chini ya kocha raia wa Uganda, Charles Lukula.

Chanzo: Mwanaspoti