Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens kuvaana na Yanga Princess kesho

Yanga P NA SIMBA Queens Simba Queens kuvaana na Yanga Princess kesho

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya wanawake Simba Queens, kesho Desemba 22, 2022 wanatarajia kushuka dimbani Benjamin Mkapa jijini Dar kuwakabili watani wao wa jadi, Yanga Princess.

Simba Queens ambao ni mabigwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake, wanakwenda kucheza mchezo huo wa raundi ya tatu mara baada ya kucheza michezo miwili ya awali.

Kwenye michezo hiyo, wa kwanza alikipiga na JKT Queens akapoteza kwa bao 2-1 kisha akakutana na The Tigers Queens na kuibuka na ushindi wa bao 4-0.

Kwa upande wa Yanga Princess, wao walianza raundi ya kwanza kwa kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess kisha raundi ya pili wakaibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Mkwawa Queens.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live