Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens, kiroho safi

Simba Queens 7 0 Wachezaji wa Timu ya Simba Queens

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Baobab Queens umeiwezesha Simba kupanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kwa mara ya kwanza msimu huu ikiiengua JKT Queens iliyoonekana kukimiliki kiti hicho kwa muda mrefu.

Mabao ya mawili ya Vivian Aquino na mengine ya Opah Clement na Jentrix Shikangwa yalitosha kuipa Simba pointi 19 baada ya mechi nane, ikiiacha JKT ikiporomoka hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 18 na Yanga Princess inafuata na pointi 17.

Simba kama ilivyo kwa JKT, Yanga, Fountain Princess na Ceasia Queens zenyewe zimesaliwa na mechi moja moja kukamilisha duru la kwanza.

Huo ulikuwa ushindi wa sita kwa timu hiyo kati ya mechi nane, ikifunga mabao 25 na kufungwa matano na kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Lukula alisema kwa sasa roho yake ipo kwatu kwani anaona kasi imeongeza maradufu baada ya kuongeza majembe matatu wenye uzoefu, Mwanahamis Omary ‘Gaucho’, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Danai Bhobho.

Lukula alisema kikosi chake kimekuwa kipana kutokana na wingi wa wachezaji wenye uzoefu ambao wanampa machaguo kuwatumia kulingana na mechi husika.

Alisema Gaucho ana kipaji hasa timu inaposhambulia kutokana na uzoefu aliyokuwa nao amekuwa akifanya kazi ya kuongoza wenzake na anasaidia pindi anapokuwa kiwanjani na Asha hajatumika muda mrefu anakosa utimamu wa mwili ila mzunguko wa pili ataisaidia timu zaidi.

“Ukiangalia baada ya kutoka kwenye Ligi ya Mabingwa ya wanawake hatukuwa na muda wa kupumzika kila mwisho wa wiki tunacheza mechi pengine ilichangia hiyo kuanza vibaya ikiwemo kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya JKT Queens,” alisema Lukula.

Unadhani nani anaweza kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu?

Chanzo: Mwanaspoti