Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens kazi bado

Simba Queens Job Kikosi cha Simba Queens

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Pamoja na kutwaa taji la ubingwa wa Cecafa, kocha mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma amesema bado ana kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha timu inafanya vizuri kwenye mashindano makubwa yaliyo mbele yao.

Simba Queens imepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Morocco.

Wekundu hao ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kwa misimu mitatu mfululizo, waliweka heshima na kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kutwaa taji la Cecafa baada ya kuifunga She Corporates ya Uganda.

Simba kwa kubeba ubingwa huo sasa itashiriki Ligi ya Afrika itakayofanyika Oktoba, mwaka huu itakayoshirikisha timu nane wakiwamo mabingwa watetezi Mamelodi na mwenyeji Far Rabat.

Nkoma alisema amefurahishwa kutwaa taji hilo na kuwa miongoni mwa timu zilizoleta msisimko wa mpira, lakini bado ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na upungufu aliouona.

“Yalikuwa mashindano mazuri kwetu, yametujengea kujiamini na yametoa kipimo kikubwa kuelekea mashindano ya kimataifa. Nina kazi ya kufanya kwa sabau kuna upungufu nimeuona,” alisema kocha huyo.

“Nina muda wa kutosha kabla ya kwenda Morocco. Nitahakikisha nasawazisha makosa yaliyojitokeza kwa lengo la kuendeleza ubora hadi kwenye mashindano makubwa tunayokwenda kushiriki.”

Wakati kocha huyo akifunguka hayo, kocha wa zamani wa Simba Queens, Matty Diola aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi huku akisema kuwa ni mwanzo mzuri kuelekea kwenye mashindano makubwa yaliyo mbele yao.

“Kupata mechi za kimataifa za mashindano kumewajengea uzoefu na ukomavu kuelekea michuano mikubwa iliyo mbele yao. Nina imani kubwa na kocha pamoja na wachezaji na natarajia mwendelezo mzuri kuelekea mashindano hayo,” alisema.

“Kupitia mashindano hayo kuna kitu kimeongezeka kwa wachezaji na kwa upande wa kocha. Naamini kuna ubora na upungufu kauona akiufanyia kazi timu inaweza kuiwakilisha nchi vizuri na kufika mbali.”

Chanzo: Mwanaspoti