Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens dimbani leo kusaka mshindi wa tatu

MSHINDI WA TATU SIMBA Kikosi cha Simba Queens kikifanya mazoezi mepesi kabla ya mchezo

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kukwama katika hatua ya Nusu fainali kwa kutolewa na timu ya Vihiga Queens katika mashindano ya CAF Womens Champions League 2021 Qualifiers.

Timu ya Simba Queens leo itashuka dimbani kuwavaa Lady Doves wa Uganda katika mechi ya kumsaka mshindi wa tatu.

Kocha wa Simba Hababuu Omar amesema timu yake imejiandaa vyema na wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa saba za mchana katika uwanja wa Kasarani, Nairobi nchini Kenya.

Simba Queens na Lady Doves wanakutana kwa mara ya pili katika mashindano haya baada ya mchezo wa kwanza kuwakutanisha katika hatua ya makundi na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.

Rais wa TFF na CECAFA Wallace Karia, amewatembelea wachezaji wa Simba Queens kuwatakia kheri katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live