Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens: Tunakwenda Ligi ya Mabingwa kushindana siyo kushiriki

DSC 6921 Kocha wa Simba Queens, Charles Ayiekoh Mbuzi

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba Queens, Charles Ayiekoh Mbuzi amefunguka mambo mengi na Global Publishers mara tu baada ya kujiunga na timu hiyo ambapo Global Publishers ilipiga kambi viunga vya Bunju kwenye uwanja wa mazoezi wa Simba SC.

Alianza kuelezea jinsi viongozi wa Simba walivyoanza mchakato wa yeye kujiunga na Simba Queens hadi akamwaga wino.

“Mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Simba Queens, uongozi wa Simba ulipendezwa na uwezo wangu ambapo meneja Selemani Makanya alinipa mwaliko kukutana kuweza kuongea”

“nilivutiwa na jinsi walivyoheshimu uwezo wangu na kukubali mahitaji yangu ambayo niliyapendekeza, tulikubaliana kuwa kama yatatimizwa nitajiunga nao, ikawa hivyo na ndio maana nipo hapa”

Kuhusu mapokezi na wasaidizi aliowakuta siku ya kwanza mazoezini pamoja na wachezaji

“Leo ndio siku ya kwanza mimi kuwa hapa, kila Kitu niliwachia wao kiutawala ili na mimi nijifunze jinsi wanavyoendesha shughuli za hapa na ndipo na mimi niweze kupandikiza yangu kuanzia mazoezi yajayo nione vya kuongeza na kupunguza kulingana na falsafa zangu”

“Nimeona ni waalimu wazuri ambao kama tutashirikiana vizuri dhima yetu itatimia na kutimiza lengo letu la kwenda kushindana Morocco na sio tu kushiriki”

Kuhusu wachezaji wa Simba Queens aliowakuta mazoezini

“wengi ninawajua vizuri, nimepata bahati ya kuwafuatilia kwenye mashindano tuliyokua tukikutana, niweke wazi kuwa moja kati ya vitu vilivyonivutia nini aina ya wachezaji waliopo hapa, Wana viwango vizuri sana na naamini wana viwango bora kwenda kushindana Morocco, nitakachoongeza mimi ni kutumia uzoefu wangu kuwajenga kuwa kitu kimoja kuanzia nje na ndani ya uwanja na badala ya kuwa mchezaji mmoja mmoja iwe timu kwa maana ya Simba Queens”

“Ahadi yangu kwa wana Simba kwa ujumla ni ushirikiano, kila mtu afanye kwa uwezo wake ili dhima yetu iweze kutimia kwa pamoja kuisaidia Simba Queens kuwa na msimu bora kule Morocco na ligi ya ndani, kiongozi afanye kwa kiwango chake, mashabiki wafanye kwa kiwango chao, wachezaji wafanye kwa kiwango chao sisi benchi la ufundi tutafanya kwa kiwango chetu pia, naimani Simba Queens itatimiza malengo yake tukiwa hivi” alimaliza kocha huyo

Ayiekoh ni kocha mwenye wasifu bora nchini Uganda kwani amewahi kufundisha timu kubwa kama URA,Vipers na Kwenye soka la wanawake ni msimu wake wa kwanza na amebeba ubingwa wa ligi ya ndani na She Corporate huku akiwasaidia kufika fainali ya CECAFA ambapo walifungwa na Simba Queens.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live