Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens, JKT Queens mechi ya kisasi

Simba Queens 2023 Simba Queens

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna neno litakalofaa kulitaja zaidi ya 'vita', pindi unapoelezea mchezo raundi ya pili wa Ligi Kuu Bara kwa upande wa wanawake, ambao utawakutanisha wenyeji, JKT Queens dhidi ya Simba Queens katika Uwanja wa Mej Isamhuyo, Dar es Salaam kesho.

Mchezo huo, utakuwa wa vita mbili kubwa, ambapo ni kisasi kwa upande wa Simba Queens ambao walifungwa mabao 2-1 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Mo Simba Arena uliopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Vita ya pili, ni kusaka uongozi wa ligi ambapo kwa sasa timu hizo zinatofautiana alama moja, Simba wakiwa kileleni na pointi zao 22 wakati JKT wakiwa wanashika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama 21, hivyo timu yoyote itakayoshinda itakaa kileleni.

JKT Queens wakati wa mapumziko ya ligi walikwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi na wamerejea jana, Jumanne wakati Simba wao waliendelea kubaki Dar es Salaam wakijiandaa pia.

Mechi nyingine ambazo zitachezwa kesho, Jumatano ni Baobab Queens watakaokipiga dhidi ya Aman Queens kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku Ceasiaa wakicheza na Alliance Girls kwenye Dimba la   Chuo cha Mkwawa Iringa.

Yanga Princess wao watakuwa na kibarua kinachofanana na Simba Queens, kwani watakuwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi yaFountain Gate Princess.

Hawa nao wana vita ya alama na kisasi, Yanga Princess walipoteza kwa bao 1-0 wakiwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, hivyo watahitaji kulipa.

Hata hivyo, kubwa ni alama tatu, wakati huu timu hizo zikiwa zinafanana alama baada ya kila moja kujikusanyia pointi 20, lakini Fountain Gates wakiwa nafasi ya tatu na Yanga Princess ya nne kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufugwa.

Mechi nyingine itakuwa ni Mkwawa Queens na The Tigers Queens katika Uwanja wa Chuo cha Mkwawa Iringa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live