Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Prisons, Singida zaweka rekodi

Singidaa+pic Simba, Prisons, Singida zaweka rekodi

Mon, 27 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver Albert MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Simba, Prisons na Singida United zimeweka rekodi tofauti kwenye msimu wa ligi 2019/20 uliomalizika jana Jumapili.

Ligi hiyo imekuwa mbaya kwa Ndanda yenye pointi 41, Lipuli (44) na Alliance(45) ambazo zimeungana na Singida United kushuka daraja moja kwa moja huku Mbao yenye pointi (45) na Mbeya City(45) zikipata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano na kama zitapoteza nazo zitashuka daraja na zikishinda zitaendelea kusalia kwenye ligi msimu ujao.

Simba imekuwa timu pekee iliyoshinda mechi nyingi kwenye ligi hiyo ikiwa imeshinda michezo 27 ikifuatiwa na Azam iliyoshinda 20 wakati Yanga ni ya tatu kwa kushinda michezo 19.

Wakati Simba ikiwa kinara wa kushinda mechi nyingi, Singida United ambayo tayari nimeshuka daraja imekuwa ndio timu pekee iliyoshinda michezo michache na kupoteza mingi msimu huu.

Timu hiyo imeshinda michezo minne tu katika mechi 38 ilizocheza msimu huu huku ikipoteza michezo 28, ikifuatiwa na KMC na Lipuli ambazo zilipoteza michezo 18 kila mmoja.

Maafande wa Prison wao wameweka rekodi ya kuwa timu iliyopata sare nyingi msimu huu, ikiwa imetoka sare michezo 19 ikifuatiwa na Yanga na JKT Tanzania ziliyopata sare michezo 15 kila moja huku Biashara United na Ndanda zikivuna sare 14 kila mmoja.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz