Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Pona pona ya Jwaneng wasilete timu uwanjani

Simba Scaled Simba: Pona pona ya Jwaneng wasilete timu uwanjani

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imewataka mashabiki wake kutokuwa na hofu katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kwani ina imani itafanya vizuri na kuingia hatua ya robo fainali.

Licha ya kukiri ubora wa Jwaneng Galaxy na pia ugumu wa mechi hiyo, Simba inayoshika nafasi ya pili kwenye kundi B imesema kuwa mashabiki watarajie furaha katika mechi hiyo.

Beki na nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala' alisema kuwa mchezo wa mwisho umekaa kimtego kwao lakini wana imani watapata ushindi na kusonga mbele.

"Itakuwa ni mechi ngumu na itakuwa ni mechi ya kuamua hatima yetu katika michuano hii lakini uzuri ni kwamba katika hizi mechi za kuamua kwenda robo fainali mara nyingi tumekuwa tukifanya vizuri.

"Tutaendelea kuwasikiliza walimu wetu nini wanahitaji kuhakikisha kwamba mchezo huo tunashinda. Hiyo ni mechi yetu muhimu, hiyo ni mechi yetu sote, naamini mashabiki watajitokeza kwa wingi kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri.

"Tunaingia katika mechi hiyo kwa tahadhari kuhakikisha tunafanya vizuri. Timu yoyote ikiwa ipo katika mechi hizi za Ligi ya Mabingwa ni nzuri na sisi tunawafahamu, hivyo tutajipanga," alisema Tshabalala.

Kocha Abdelhak Benchikha alisema kuwa matokeo ya ushindi ndio wanayahitaji kwenye mechi ya mwisho kwa vile ndio yatawapeleka robo fainali.

"Tuna njia moja tu ya kufanya ambayo ni kupata ushindi. Tutacheza kwa ajili ya kushinda na tunatuma ujumbe kwa mashabiki wetu waje uwanjani kutupa sapoti.

"Tumecheza mechi nzuri Ivory Coast. Tulipoteza nafasi moja nzuri ya kufunga hatukuitumia. Kwa sasa akili yetu tunaielekeza katika mechi inayofuata ambayo naamini tutapata ushindi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live