Mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga, Fiston Mayele aliyefunga mabao 16 kwenye ligi anatarajiwa kukwaa vigingi vitatu Agosti 13, kwenye mchezo dhidi ya Simba.
Nyota huyo anashikilia rekodi ya kuwatungua Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa msimu wa 2021/22 wakati huo alipokuwa chini ya beki bora wa msimu Henock Inonga raia wa DR Congo.
Agosti 13 Mayele ambaye ana uzoefu na mechi za Simba na Yanga kwa kuwa amecheza mechi nne kati ya hizo mbili za ligi, moja ya Ngao ya Jamii pamoja na ile ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza mchezo ujao.
Kisiki cha kwanza ambacho atakutana nacho ni Inonga ambaye rekodi zinaonyesha kuwa wamekuwa wakionyeshana umwamba kila wanapokutana kwenye Kariakoo Dabi.
Kisiki cha pili itakuwa ni ingizo jipya ndani ya Simba ambaye ni beki Mohamed Ouattara aliyeonesha kiwango kwenye mchezo wa kwanza wa ushindani dhidi ya St George.
Tatu ni kiungo mkata umeme w ambaye aliibuka Simba akitokea Coastal Union iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga huku kiungo huyo akiwa ni mmoja ya wale waliokuwa kisiki kwa Mayele hivyo wanatarajiwa kukutana kwa mara nyingine akiwa na uzi wa Simba.
Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga alisema kuwa anawaandaa wachezaji wake wote kuweza kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii.