Simba imechangamsha wakazi wa kuanzia njia panda ya kwenda Turiani, Magore na Mvomero, ambao baada ya kuona linapita basi lililowabeba wachezaji walitanda barabarani na kulipungia mkono.
Walianza wakazi wa njia panda ya Turiani maarufu kama Feli, kusimamisha shughuli zao kwa muda, huku basi la timu hilo likisindikizwa na msafara wa bodaboda walioibua shangwe na kuwafanya waliokuwa majumbani kutoka kulishangilia.
Wakafuatia wakazi wa Magore ambao nao walikuwa wanalishangilia basi hilo likiwa linapita, huku wakipaza sauti kwa wachezaji wakiwataka wakashinde mechi hiyo. "Tunaraka mkirudi tuwapokee kwa shangwe la ushindani, tunawaomba kila la kheri," Kisha likafuata vaibu la shangwe na miluzi.
Walimalizia mashabiki wa Mvomero ambao walikuwa wanapunga mikono na kuwatakia kheri wachezaji hao ili kuifunga Mtibwa Sugar, mechi inayopigwa Uwanja wa Manungu.