Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba , Luis Miquissone mambo fresh!

Jose Luis Miquissoneeee Luis Miquissone

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba Sc juzi iliendelea kutambulisha mastaa wapya wakati kundi la mwisho la wachezaji likijianda kupa kwenda kambini jijini Ankara, Uturuki, lakini taarifa njema kwa mashabiki na wapenzi ni dili la winga wa zamani wa timu hiyo, Luis Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri kukamilika.

Ndio, kwa sasa ni rasmi Luis aliyeuzwa na Simba misimu miwili iliyopita atavaa uzi wa mwekundu na mweupe kama aliokuwa akivaa Al Ahly, lakini safari hii ni kwa mara nyingine akiwa na Simba baada ya klabu hiyo ya Msimbazi kukamilisha dili la kumrejesha kikosini kwa mkopo.

Mwanaspoti kama kawaida, liliwajulisha jana kwamba dili hilo lilikuwa limefikia patamu na jana limejiridhisha kwamba mchezaji huyo ataichezea Simba kwa msimu ujao baada ya kukamilisha kila kitu kuhusu mchezaji huyo raia wa Msumbiji kurejea Msimbazi akitokea Al Ahly.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Simba ni kuwa,  mabosi wa klabu hiyo, wamemalizana na wenzao wa Al Ahly ili kumrejesha Luis kwa mkopo na tayari wamempa mkataba wa miaka miwili na anatarajia kuungana na Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' pamoja na wenzake kambini Uturuki.

Mmoja wa vigogo wa klabu hiyo ya Simba, aliliambia Mwanaspoti kuwa, winga huyo hatari na kipenzi cha mshabiki wa Simba ataenda kuinogesha kambi ya timu hiyo wiki ijayo baada ya kila kitu kuhusu dili lake kukamilika.

Luis aliyesajiliwa na Simba mwaka 2020 akitokea UD Songo ya Msumbiji na hadi anaondoka Msimbazi miwili miwili iliyopita alikuwa amefunga mabao tisa na asisti 15 na sasa anajiunga na Simba akitokea Abha aliyokuwa akiichezea kwa mkopo baada ya kutolewa na Al Ahly.

"Tumedhamiria kunyakua mataji msimu ujao, mashabiki watulie mambo mazuri yanakuja, Simba inasajili kikosi cha kazi, tayari wamewaona wengine tuliowatangaza na uwezo wao ni mkubwa kutokana na rekodi walizoziacha kwenye timu walizotokea," alisema kigogo huyo na kuongeza;

"Kambi ya Uturuki itanoga itakuwa na wachezaji wote wapya na wa zamani, kocha atapata wakati mzuri wa kuwasoma wachezaji wake na kuhusu Luis ni uhakika ataichezea timu yetu na atajiunga na timu huko huko Ankara kuanzia Julai 20, kwani mambo yamekamilika."

Kutua kwa Luis kunaifanya Simba iongeze nguvu eneo la mbele ambalo tayari lina maingizo mawili mapya akiwamo Aubin Kramo kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast na Willy Onana aliyekuwa Rayon Sports ya Rwanda na jana ilimtambulisha Fabrice Ngoma aliyekuwa Al Hilal ya Sudan.

Mbali na hao, Simba kikosini ina Kibu Denis, Peter Banda, Moses Phiri, John Bocco, Saido Ntibazonkiza na Pape Ousmane Sakho aliye mbioni kuondoka klabuni hapo kwenda Ufaransa.

Chanzo: Mwanaspoti