Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Kwa Vipers! shughuli mbona imeisha

Simba SC Vipers Gh Wachezaji wa Simba wakipongezana katika mchezo dhidi ya Vipers Uganda

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba inajiandaa kushuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam Jumanne ijayo (Machi 7) kuvaana na Vipers ya Uganda katika mechi ya Kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mabosi wa klabu hiyo wakitamba kuwa, wapinzani hao watawakalisha mapema tu.

Simba iliifunga Vipers kwa bao 1-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa wikiendi iliyopita na Jumanne watarudiana ili kutoa picha halisi baina yao juu ya kukata tiketi ya kwenda robo fainali ya michuano ya msimu huu.

Simba ipo nafasi ya tatu na pointi tatu kundini, ikiwa ni mbili zaidi na ilizonazo Vipers inayoburuza mkiani, huku Ac Horoya ya Guinea ikiwa ya pili na pointi nne huku vinara wakiwa ni Raja Casablanca ya Morocco ikiongoza kwa pointi tisa.

Akizungumza mapema leo jijini Dar, Afisa habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kikosi hicho kimeingia kambini leo MO arena kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao na Vipers FC utakaochezwa machi 7 mwaka huu saa 1 kamili usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed ameyasema hayo leo Ijumaa wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba wameingia mazoezini mapema kutokana na umuhimu wa mchezo huo.

Aidha ameongeza kwamba mechi itakuwa ngumu kwa upande wao huku akieleza ya kwamba kwa Vipers kuondoka na alama 3 kwa mkapa itakuwa ngumu.

" Siku hiyo tumeipa jina la "Jumanne ya wenye nchi" kwa maana ya kwamba wananchi wapo ila sisi ndio tutaishika nchi kwa mkapa hii mechi inaenda kuamua hatma yetu wanasimba", Alisema Ahmed na kuongeza kuwa

" Itakuwa aibu kubwa kama wanasimba kama tutaishia hatua ya mtoano hii ni michuano yetu jumanne tunampiga vipers na kuiona hatua ya robo fainali kule".

Pia ameeleza namna hamasa ya sasa kwa mashabiki itakuwa na utofauti na waliozoea siku ya jumapili asubuhi Coco Beach kutakuwa na shughuli ikiambatana na michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu.

"Tumekuwa tukizunguka na kwenye maeneo mbalimbali ya wazi tukiwa na kispika, kutangaza mechi yetu, mechi hii imekuja na kitu cha utofauti na chenye mvuto zaidi kinaitwa 'wenye nchi beach party' hii itakuwa jumapili kwenye ufukwe wa coco". Alisisitiza Ahmed

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mechi hiyo huku ikiwa mara ya kwanza kwake tangu aapishwe.

Vipers FC watawasili nchini jumatatu asubuhi huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa nyumbani kwake na Simba kwa bao 1-0 nchini Uganda wikiendi iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live