Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, JKT Tanzania ni vita vya heshima

Simba Vita Pic Data Simba, JKT Tanzania ni vita vya heshima

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kinashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Simba katika mchezo huu wanahitaji huku wakicheza kwa tahadhari kwa timu hizi mbili zina historia ya kusumbuana katika michezo yao.

Msimu uliopita, katika mchezo uliofanyika Agosti 29, JKT Tanzania wakiwa wenyeji walifungwa na Simba mabao 3-1 na katika mchezo wa marudiano uliochezwa Februari 7, Simba wakiwa wenyeji walifungwa 1-0.

Katika msimu huu, Simba iliichapa JKT Tanzania wakiwa nyumbani kwa mabao 4-0 mchezo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Oktoba 4.

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema katika msimu huu kila mechi kwao ni fainali kwani wanahitaji makombe yote.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz